| 
 
Watanzania
              wana simulizi za kusisimua kuhusu asili yao. 
              Hapo zamani za kale, kutokana na uso wa ardhi kutokuwa
              mgumu, ardhi ilipasuka na kusababisha Bonde la Ufa ambalo
              linatanda kuanzia kusini mwa Yemen kupitia nchi za Afrika ya
              Mashariki ikiwemo Tanzania, hadi Ziwa Nyasa na kugawanyika
              magharibi kati ya Tanzania na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. 
              Moja ya sehemu mashuhuri sana katika Bonde hilo ikatokea
              ndiyo chimbuko la binadamu.  Binadamu
              wa awali anafanana na nyani na kwamba fuvu lake na nyayo
              ziligunduliwa na familia ya Leakeys hapo mwaka 1959 na 1979. 
              Ushahidi huu ambao ni matokeo ya uvumbuzi wa elimukale
              kuhusu binadamu wa kwanza ulipatikana katika Bonde la Olduvai na
              Laetoli.  Maeneo hayo
              yalikuwa baadhi ya makazi ya ukoo safu wa kisasa (homo habilis na
              homo sapiens), wazee wa kitanzania ambao waliweza kufikiri na
              kutengeneza vifaa vinavyotokana na mawe. 
              Mabaki muhimu ya vifaa na mifupa vilivyoachwa na aina ya
              binadamu, vinakadiriwa kuwa na umri wa miaka milioni moja na
              sabini na tano elfu.  Aidha,
              ushahidi kamahuo umechimbuliwa kwenye maeneo ya kihistoria huko
              Isimila katika Nyanda za Juu za Kusini ambako vifaa vya kale,
              vijulikanavyo kama shoka vinaweza kuonekana leo. 
              Michoro kwenye mapango ya Kondoa-Irangi iliyochorwa na babu
              zetu hao na dalili za shughuli za uhunzi na umwagiliaji maji
              mashamba ni ushahidi mwingine wa kuwepo kwa dalili za mtu wa
              kwanza katika Tanzania kwa wakati wa kale.  Ni vyema kusadiki na kukubali kutoka hapo ni kwamba baadhi ya
              wazao walitawanyika duniani kote na baadaye kurejea Tanzania
              kujiunga na dada na kaka zao waliobaki hapa nchini. 
              Hao sasa walirejea kama wapiganaji wakulima, wachungaji
              walowezi, wavamizi, wakimbizi, wakoloni, wafanyabiashara,
              wavumbuzi, wamisionari au watafuta watumwa. 
              Idadi kubwa ya watu hao ndiyo wanaunda jamii ya watanzania
              wa leo ikiwa ni pamoja na makabila makubwa (asilimia 99) bila
              kuwajumuisha makundi madogo kutoka  Ulaya na Asia (asilimia 1). 
              Kutokana na kukosekana kwa hali ya utulivu kama kawaida na
              mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi za jirani hivi sasa na
              hata hapo zamani, Tanzania imekuwa ni mahala pa makimbilio kwa
              wahamiaji.  Wakimbizi
              kutoka makutano ya Benini-Benne Africa magharibi, Bahr el Ghazal
              nchini Sudan na maeneo ya Shunygwaya nchini Kenya wote walihamia
              Tanzania kati ya karne ya tatu na kumi na tatu. 
              Hii leo Tanzania bado anapokea na kuwahudumia maelfu ya
              wakimbizi kutoka Burundi, Rwanda, Somalia na Jamhuri ya Demokrasia
              ya Kongo.  Hali hii
              inaleta mgongano mkubwa kwa idadi ya watu nchini, rasilimali na
              mazingira.  Idadi ya
              wakimbizi hao inakadiriwa kuwa kati ya 500,000 hadi 1,000,000. 
              Wakimbizi wamesababisha athari kubwa kwa nchi hii. 
              Kutokana na mahitaji ya chakula, maji na kuni, karibu
              vyanzo vyote vya maji na mimea ya asili ya sehemu husika na jirani
              ya kambi hizo za wakimbizi zimeharibiwa. 
              Matokeo yake ni  kwamba
              maeneo hayo yamegeuzwa kuwa maeneo yasiyokuwa na kitu, maeneo
              yaliyo katika hali ya jangwa. 
 
 
              
               
 
Mauaji,
              wizi  na aina nyingine
              za maovu yamefanywa na baadhi ya wakimbizi na hivyo kusababisha
              usumbufu kwa jamii na kutoweka kwa amani kwa baadhi ya raia wa
              Tanzania.  serikali ya Tanzania, Umoja wa Nchi za Afrika (OAU), Shirika
              la Umoja wa Mataifa la kushughulikia 
              wakimbizi (UNHCR) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto
              (UNICEF) wanajitahidi kuwarekebisha wakimbizi hao ili wakati
              muafaka ukifika warejeshwe makwao. 
 
 
              
               
 
Kwa
              jumuiya ya kimataifa suala la wakimbizi ni eneo lingine ambalo
              linahitaji msaada zaidi kwa Tanzania ili kuiwezesha kuwasaidia
              wakimbizi hao kuishi kama binadamu wengine pamoja na kusaidia
              kuleta amani kwenye nchi zao ili ziweze kuwa mahala pa kuishi. 
 
 
              
               
 
 
 
              
               
 
Hali
              ya mvuto wa mfumo ya jamii wa Tanzania ni kivutio kikubwa kwa
              masuala ya utamaduni, uchumi na utalii. 
              Hadithi za watu wa kale, ngoma za asilia na aina ya ngoma
              zinatofautiana kati ya kabila na kabila. 
              Wanapocheza, Wamakonde kuchezesha viuno vyao kwenda
              sambamba na ngoma ya “sindimba”, Wazaramo humezwa na
              maandamano ya “mdundiko”. 
              Wamaasai huruka kwa mpangilio maalum huko wakitoa 
              sauti nzito ambazo zinaweza kumwogofya simba dume! 
              Matumizi ya nyoka hai na kucheza na nyoka wakubwa kama
              chatu kunakofanywa na Wasukuma wakati wanacheza ngoma ya
              “Bugobogobo” hakuwezi kusahaulika kwa mgeni. 
              Kila kabila kati ya  makabila
              120 ya Tanzania ina ngoma yake na staili zake za uchezaji ambazo
              zinapumbaza kwa kukazia macho zinafurahisha na kuvutia kijinsia. 
 
 
              
               
 
Aina
              mbalimbali ya mavazi pia hutoa mvuto 
              wa aina yake kwa mgeni. 
              Wanaume wa Kimasai huvaa vazi ambalo halifuniki mwili wote
              huku wakitembea na mikuki, virungu na visu vikubwa. 
              Kwa upande wao, wanawake wa Kimasai hujaza tele shingo zao,
              mikono, miguu na masikio yao na vitu vya thamani vikiwemo shanga
              na hadi aina nyingine za madini. 
              Wanaume wa Kimasai hupakaza miili yao na udongo mwekundu
              uliochanganywa na mafuta yatokanayo na wanyama na husuka nywele
              zao. 
 
 
              
               
 
 
              
               
 
 
              
               
 
 
              
               
 
Wamakonde
              nao huchonga meno yao na kuchanja nyuso na miili yao taaluma
              inayotamanisha.  Wamakonde
              ni wataalam wa kuchonga vinyago vinavyoonyesha matatizo ya
              binadamu, mapambano, mapenzi, tamaa, wema, ubaya na mshikamano
              vitu ambavyo vinavutia sana na kuamsha fikra. 
 
 
              
               
 
Wakazi
              wa pwani na visiwani hupamba mikono, miguu, midomo na kucha
              kufuatana na tukio shughuli ambayo huleta mvuto mkubwa. 
 
 
              
               
 
Kati
              ya makabila ya namna ya pekee ni makundi ambayo yanakadiria
              kutoweka yaishiyo kati ya Tanzania. 
              Makabila  haya
              ni ya Wasandawe (wanahusiana na Waethopia) ambao jirani zao ni wa
              Iraqw gorowa na burungi na Wadzapi ambao pia hujulikana kama
              Watindiga na Wakangeju na Wahontetot - wanaohusiana na kabila la
              Khosa la Afrika Kusini ambao huzungumza lugha za “click”. 
              Wandorobo pia wanazungumza lugha hiyo lakini wameiga zaidi
              utamaduni wa nje ya mazingira yao.  Watanzania hao ni wa kuhamahama, wachumaji matunda, wawindaji
              wakusanyaji chakula, na wavuvi waishio katika eneo linalozunguka
              Ziwa Eyasi ambalo liko kilomita chache kutoka bonde maarufu la
              Ngorongoro.  Inasemekana
              kwamba idadi ya watu hawa kwa sasa haifikii 500 wakati mwaka 1965
              walikuwa zaidi ya 30,000. 
 
 
              
               
 
Wito
              hapa ni kuisaidia Serikali ya Tanzania kuwaokoa watu hao wasifikie
              ukingo wa kutoweka.  Kwa
              maana hiyo, maeneo yanayozunguka Ziwa Eyasi ni bora kabisa ya
              kufanyia utafiti wa kisayansi wa elimu ihusuyo habari za asili na
              maendeleo ya  binadamu
              kwa ajili ya kumbukumbu za baadaye.  Kinachojitokeza ni kwamba ni vyema kutambua kuwa huu ni
              wakati muafaka wa kufanya uchunguzi ama vile watu hao watakuwa
              wametoweka kabisa.
 | 
No comments:
Post a Comment