Tuesday, July 28, 2015

SHERIA YA BARAZA LA SANAA LA TAIFA,



          Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa
 

TANGAZO LA SERIKALI NA. 322 la tarehe 21/10/2005

SHERIA YA BARAZA LA SANAA LA TAIFA, 1984
[NA. 23 YA 1984]


 
KANUNI


 
Zimetungwa chini ya Kifungu cha 5


 
KANUNI ZA BARAZA LA SANAA LA TAIFA, 2005

  1. Kanuni hizi zitaitwa Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, 2005, na zitaanza kutumika mara baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

  1. Kwa madhumuni ya kanuni hizi na isipokuwa kama maelezo yatahitaji tafsiri nyingine;

“Baraza” maana yake ni Baraza la Sanaa la Taifa lililoundwa chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya mwaka 1984.

“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya kushughulikia Sanaa
“Kamati” maana yake ni Kamati ya Sanaa ya Mkoa au ya Wilaya
“Msajili” maana yake ni Msajili au Msajili Msaidizi wa Vikundi, Vyama au Asasi zinazojishughulisha na sanaa

  1. Kutakuwepo na Baraza la Sanaa la Taifa chini ya Baraza hilo kutaunda Kamati za Sanaa za Mikoa na za Wilaya zitakazofanya kazi za Baraza katika ngazi za Mikoa na Wilaya.

  1. katika kila ngazi, Kamati za Sanaa zitakuwa na majukumu yafuatayo:

(a)    kubeba dhamana ya kufufua na kukuza maendeleo na kuongeza utengenezaji wa bidhaa za sanaa ktika Mkoa au Wilaya, ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti wa vyombo vya muziki, nyimbo, mashairi, na ngoma za asili na mapokeo kwa lengo la kuibua na kuendeleza utamaduni wa Tanzania;

(b)   Kufanya utafiti wa maendeleo na uzalishaji wa kazi za sanaa, ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti wa viwango na thamani ya kazi za sanaa zinazofanywa katika Mikoa au Wilaya;

(c)    Kutoa huduma za ushauri na misaada ya kiufundi ambayo ni ya lazima au ya nyongeza katika kuendeleza shughuli za sanaa kwa asasi na watu mbalimbali wanaojishughulisha na kazi hizi;


Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


(d)   Kuandaa mipango na kuratibu shughuli za sanaa zinazofanywa na watu au asasi mbalimbali

(e)    Kulishauri Baraza juu ya mambo yahusuyo maendeleo na ukuzaji wa kazi za sanaa katika Mikoa au Wilaya na tTaifa kwa ujumla;

(f)    Kutoa na kuimarisha njia za vifaa vya mafunzo kwa ajili ya watu wanaojishughulisha, walioajiriwa na watakaoajiriwa katika vyombo vya kazi za usanii;

(g)   Kushughulikia na kuzisaidia asasi au mtu yeyote katika uingizaji na ununuzi wa bidhaa za sanaa kutoaka nchi za nje, pamoja na uuzaji wa kazi za sanaa nje ya nchi

(h)   Kuhimiza maendeleo ya kazi za sanaa kwa kuandaa na kufanya au kusimamia maonyesho, ngoma, kuendesha warsha, semina na mashindano baina ya wasanii mbalimbali

(i)     Kufanya jingine lolote ama kwa maelekezo ya Baraza au kwa faida ya maendeleo ya sanaa katika Wilaya, Mkoa na Taifa kwa jumla

  1. Zitaundwa kamati katika Baraza, na kamati ndogo katika Kamati za Sanaa za Mikoa na za Wilaya ili kurahisisha utekelezaji wa kazi za Baraza kwa ujumla wake. Kamati hizo ni:

  1. Kamati ya Utendaji ya Baraza ambayo itaundwa na Wajumbe wafuatao;

(a)    Mwenyekiti wa Baraza ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati;

(b)   Katibu Mtendaji wa Baraza ambaye atakuwa Katibu wa Kamati;

(c)    Makamu Mwenyekiti ambaye atachaguliwa na Wajumbe kutoka miongoni mwao;

(d)   Wajumbe wane (4) watakaochaguliwa na Baraza kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Baraza;

(e)    Mhasibu wa Baraza (Hapigi Kura)



Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


  1. Kamati ya Utendaji itakuwa na majukumu yafuatayo:

(a)    Kutekeleza maazimio na shughuli zote za Baraza;

(b)   Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Utamaduni;

(c)    Kupanga tarehe za mikutano ya Baraza;

(d)   Kuandaa na kuendesha Semina na Warsha kwa wasanii, viongozi wa vikundi, asasi au watu binafsi wanaojishughulisha na kazi za sanaa;

(e)    Kuandaa orodha na kuweka kumbukumbu za wasanii mahiri wa fani mbalimbali za Sanaa;

(f)    Kushughulikia mambo mengine yote yenye manufaa kwa Baraza na maendeleo ya Sanaa kwa jumla

  1. Kamati ya Utafiti na Ufundi ya Baraza, au Kamati Ndogo ya Kamati ya Sanaa itakuwa na wajumbe wafuatao:

(a)    Wajumbe wasiozidi wanane (8) wenye utaalamu wa fani mbalimbali za sanaa watakaochaguliwa na Baraza au Kamati kutoka miongoni mwa Wajumbe wa Baraza au Kamati;

(b)   Ofisa wa Baraza au Katibu wa Kamati ya Sanaa atakuwa Katibu wa Kamati hii

  1. Kamati ya Utafiti na Ufundi itakuwa na majukumu yafuatayo:
(a)    Kuchambua na kuweka takwimu thabiti ya mahitaji ya kuendeleza sanaa mbalimbali;

(b)   Kuratibu kazi za utafiti wa sanaa;

(c)    Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Kamati ya Utendaji kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ya sanaa;

(d)   Kuainisha sheria na kanuni za mashindano mbalimbali

(e)    Kutengeneza programu ya Maendeleo ya Sanaa



Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)



  1. Kamati ya Fedha, Mipango na Masoko ya Baraza, au Kamati Ndogo ya Kamati ya Sanaa itakuwa na Wajumbe wafuatao:

(a)    Makamu Mwenyekiti wa Baraza au kamati atakuwa ndiye Mwenyekiti

(b)   Mhasibu au Mweka Hazina wa Baraza au kamati atakuwa Katibu

(c)    Wajumbe wengine watatu (3) watakaochaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe wa Baraza au Kamati.

  1. Kamati ya Fedha, Mipango na Masoko itakuwa na  majukumu yafuatayo:
(a)    Kubuni njia nzuri ya kuliingizia mapato Baraza
(b)   Kuchambua taarifa za mapato na matumzi ya fedha
(c)    Kusimamia miradi ya Baraza au Kamati
(d)   Kubuni mbinu za kupata masoko ya kazi za sanaa
(e)    Kufanya mengineyote kwa maelekezo ya Kamati ya Utendaji

  1. – (1) Kutakuwa na kamati fya Sanaa ya Mkoa kwa kila Mkoa ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao:

(a)    Mwenyekiti atakuwa ni katibu Tawala wa Mkoa

(b)   Katibu wa Kamati atakuwa Ofisa Utamaduni wa Wilaya ambayo ni makao makuu ya Mkoa;

(c)    Maofisa Utamaduni wa Wilaya zote zinazounda Mkoa watakuwa ni wajumbe

(d)   Wajumbe wengine wasiozidi watatu (3) watakaoteuliwa na Mkuu wa Mkoa kwa kadri watakavyona inafaa

(e)    Mweka Hazina atakayechaguliwa na wajumbe kutoka miongoni mwao

(f)    Mjumbe mmoja mmoja kutoka kila chama cha Sanaa cha Mkoa

  (2) Wajumbe wote waliotajwa katika kanuni ya 12 watateuliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa

  (3) Mkuu wa Mkoa anaweza kuteua mjumbe kujaza nafasi iliyoachwa wazi kutoakana na mjumbe kujiuzulu, kuachishwa, kufariki, kufukuzwa au sababu nyingine.
Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


  (4) Wajumbe watakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu (3) na wanaweza kuteuliwa tena.

  1. –(1) Kutakuwa na kamati ya Sanaa ya Wilaya kwa kila wilaya ambayo itakuwa na Wajumbe wafuatao:-

(a)    Mwenyekiti atakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya/Mji au Manispaa;

(b)   Katibu wa Kamati atakuwa Afisa Utamaduni wa Wilaya, Mji au Manispaa;

(c)    Wajumbe wengine watatu (3) watakaoteuliwa na Mkuu wa Wilaya kwa kadri atakavyoona inafaa

(d)   Mweka Hazina atakayechaguliwa na Wajumbe kutoka miongoni mwao

(e)    Mjumbe mmoja mmoja kutoka kila Chama cha Sanaa cha Wilaya

  (2) Wajumbe wote waliotajwa katika, Kanuni 13 watateuliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya.

  (3) Mkuu wa Wilaya anaweza kuteua Mjumbe kujaza nafasi iliyoachwa wazi kutokana na Mjumbe kujiuzulu, kuachishwa, kufariki, kufukuzwa au sababu nyingine.

  (4) Wajumbe watakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu (3) na wanaweza kuteuliwa tena.

  1. Kutakuwa na kamati Ndogo ya Utendaji kwa kila Kamati ya Sanaa ya Mkoa au Wilaya itakayokuwa na wajumbe wafuatao:

(a)    Mwenyekiti wa Kamati ya Sanaa atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji

(b)   Katibu wa Kamati ya Sanaa atakuwa Katibu wa Kamati ya Utendaji

(c)    Makamu Mwenyekiti wa Kamati

(d)   Mwenyekiti wa Kamati ya Utafiti na Ufundi


Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


(e)    Mwendyekiti wa Kamati ya FEdha, Mipango na Masoko

(f)    Wajumbe wengine watatu (3) watakaochaguliwa na Kamati ya Sanaa kutoka miongoni mwa Wajumbe wake.

(g)   Mweka Hazina wa Kamati

  1. –(1) Kamati ya Sanaa ya Mkoa au ya Wilaya itafanya Mkutano wake mara moja kwa mwaka au wakati wowote kwa kikao cha dharura.
(2) Kamati ya Utendaji ya Baraza, na Kamati Ndogo ya Utendaji ya Kamati yaSanaa itakutana angalau mara moja kwa kila miezi miwili.
(3) Kamati nyingine zote za Baraza, na Kamati Ndogo nyingine zote za Kamati za Mikoa na Wilaya zilizotajwa katika Kanuni ya 5 zitafanya vikao vyake kwa maelekezo ya Kamati ya Utendaji au kulingana na mahitaji, lakini si chini ya mara moja kwa miezi mitatu.

  1. -(1) Vikao vyote vya Baraza na Kamati, kwa mujibu wa Kanuni hizi,, vitafanyika endapo idadi ya wajumbe wote waliohudhuria haipungui nusu ya idadi ya wajumbe wote wanaohusika;

(2) Endapo Mwenyekiti aliyechaguliwa au kuteuliwa hayupo wakati wa kikao, Makamu Mwenyekiti ataongoza kikao. Endapo Makamu Mwenyekiti naye hayupo, Wajumbe watamchagua Mwendyekiti wa muda kuongoza kikao.

(3) Upigaji Kura utakuwa wa siri

(4) Mwenyekiti wa Baraza, Kamati au Kamati Ndogo atapiga kura ya uamuzi endapo kura zililingana.

  1. –(1) Kutakuwepo na Msajili wa vikundi na vyama vya sanaa takayeteuliwa na Waziri

(2) kazi ya Msajili itakuwa ni kusajili vyama, jumuia na asasi za watu binafsi zinazojishughulisha na kazi za Sanaa.

(3) Msajili atatekeleza majukumu yake kwa kusaidiwa na Wasajili Wasaidizi ambao ni Maofisa Utamaduni wa Wilaya.


Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


  1. –(1) Jumuiya, chama au asasi inayotaka kujishughulisha na kazi za sanaa itatakiwa iwe imesajiliwa.

(2) Hakuna chama au asasi itakayoruhusiwa kuendesha shughuli za sanaa bila kusajiliwa

  1. –(1) Jumuiya au mtu yeyote atakayetaka kusajili asasi yake ya kushughulika na kazi za sanaa atapeleka maombi yake kwa Msajili.

Msaidizi aliyeko katika Wilaya ambayo ni makao Makuu ya chama au asasi hiyo, Maombi hayo yaambatanishwe na:

(a)    Mhutasari wa kikao cha wanachama kilichopitisha uamuzi wa kuandaa Chama hicho au kikundi hicho, au uthibitisho wowote wa kuonyesha uhalali wa kumiliki asasi inayojishughulisha na kazi za sanaa;

(b)   Nakala tatu za katiba ya chama au mwongozo wa kikundi au asasi

(c)    Taarifa nyingineyoyote kama itakavyoelekezwa na Msajili Msaidizi au Msajili.

(2) Baada ya Msajili Msaidizi kupokea maombi hayo, atatoa fomu maalumu kwa mwombaji ambaye atazijaza na kasha kuzirejesha kwa Msajili Msaidizi. Baada ya hatua hiyo, Msajili Msaidizi atatuma nyaraka zote za maombi hayo kwa Msajili

(3) Msajili akishapokea maombi ya usajili, atawajulisha wahusika kuhusu ama kukubaliwa au kukataliwa maombi yao katika kipindi kisichozidi siku 14 kuanzia tarehe ya kupokeelewa maombi hayo.

  1. -(1) Msajili anaweza kukataa maombi yoote ya usajili ikiwa:
(a)    Jina la chama au kikundi kinachoomba kusajiliwa linafanana na jina la Jumuiya nyingine iliyosajiliwa na Msajili wa Sanaa au mamlaka nyingine yoyote

(b)   Kazi za chama kinachooomba kusajiliwa zinakiuka sheria za nchi ama zinaweza kuathiri utekelezaji wa Sera za Serikali;

(c)    Anaona kuwa malengo ya Chama kinachoomba kusajiliwa yanaweza kuhatarisha usalama na kuvuruga amani miongoni mwa jamii kwa  ujumla na hivyo kuathiri maendeleo ya kazi za sanaa;


Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


(d)   Kwa maelekezo ya Waziri

(2) Kila katiba au mwongozo wowote wa chama, kikundi au mtu binafsi    
     unatakiwa kuweka wazi mambo muhimu yafuatayo:

(a)    Jina la chama

(b)   Wamiliki wa chama au asasi

(c)    Anuani kamili, ikiwa ni pamoja na mahali, sanduku la posta, namba ya simu na kadhalika

(d)   Madhumuni ya Chama au asasi

(e)    Utaratibu wa uendeshaji wa shughuli za chama na kazi za sanaa kwa ujumla wake

(3) Chama au kikundi chochote kitakachofanya marekebisho ya kifungu chochote cha katiba au  mwongozo wake, kitatakiwa kupata idhini kwa Msajili kabla ya kifungu hicho kuanza kutumiwa.

  1. –(1) Endapo Msajili atakataa maombo yoyote ya usajili au ya kubadilisha kifungu chochote cha katiba, mwombaji anaweza kukata rufaa kwa Waziri dhidi ya uamuzi wa Msajili katika kipindi kisichozidi siku 21 tangu maombi yakataliwe.

(2) Uamuzi wa Waziri ni wa mwisho

  1. –(1) Kila chama kitatakiwa kuwasilisha kwa Msajili taarifa ya utekelezaji wa shughuli zake za mwaka mzima kati ya tarehe 1 na 30 ya mwezi Juni ya kila mwaka.

(2) Kila chama kitatakiwa kuwasilisha kwa Msajili taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka ya fedha zake kati ya tarehe 1-30 ya Juni ya kila mwaka

  1. –(1) Msajili, kwa sababu maalumu au kwa kadri atakavyoona inafaa, anaweza kukitaka chama kuwasilisha kwake taarifa yoyte inayohitajika kwa kutoa taarifa isiyopungua siku 30.

(2) Msajili, anaweza kuamuru kiongozi yeyote wa chama kufika ofisini kwake ili kutoa taarifa inayojitajika au kupokea maelekezo kwa kadri atakavyoona inafaa, ili mradi wito huo uwe umetolewa si chini ya siku saba kabla ya tarehe ya kutwa.

Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


(3) Msajili anaweza akatembelea eneo lolote na kwa wakati wowote kuona utekelezaji wa kazi za sanaa baada ya kutoa taarifa kwa chama kinachohusika

  1. –(1) Wakati wowote, Msajili anaweza akafuta usajili wa asasi, kikundi au chama chochote kinachoshughulikia sanaa endapo atabaini kuwa:

(a)    Chama, asasi au kikundi hicho kinachochea uhasama miongoni mwa jamii kwa kutumia tofauti za kisiasa au udini au ubaguzi wa aina yoyote ile;

(b)   Chama, asasi au kikundi hicho kinatekeleza malengo tofauti nay ale yaliyoidhinishwa katika katiba yake

(c)    Chama, asasi au kikundi hicho kiantumika na kinaelekea kutumika kuvuruga amani na misingi ya utawala bora miongoni mwa jamii;

(d)   Chama, asasi au kikundi hicho kinavunja sheria na kukiuka kanuni zinazoongoza kazi za sanaa nchini

(2) kabla ya kufuta usajili wa chama, asasi au kikundi chohcote kutokana na sababu zilizotajwa katika kifungu 24 (1), Msajili atatoa taarifa ya kusudio la kufuta usajili na kutoa fursa kwa chama, asasi au kikundi kinachohusika kutoa sababu, katika muda usiozidi miezi mitatu, kwa ini kisifutiwe usajili.

(3) Endapo chama kinachohusika hakitaridhishwa na kusudio hilo la Msajili, chama hicho kinaweza kukata rufaa kwa Waziri dhini ya kusudio la Msajili katika kipindi kisichozidi siku 21 tangu tarehe ya kupewa taarifa. Uamuzi wa Waziri utakuwa wa mwisho.

  1. –(1) usajili wa vyama vya sanaa vya Wilaya, Mikoa na Taifa utazingatia aina za sanaa katika kila ngazi.

(2) Ili chama cha sanaa cha Taifa au Mkoa au Wilaya kiweze kusajiliwa, kitatakiwa kuwe na muundo uliowekwa bayana katika katiba yake na uliokubaliwa na wanacama wake wote au katika ngazi zake zote.

(3)  Mawakala, wakuzaji na wafanyabiashara za sanaa watalipa ada katika ngazi huzika ili kupata idhini ya kuendesha shughulizao.

(4) Mawakala, wakuzaji na wafanyabiashara za sanaa, watatakiwa kuwa na mikataba na wasanii inayotambuliwa na Baraza


Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


(5) Watumiaji wa kazi za sanaa kwa lengo la kufundishia au kutoa mihadhara wanatakiwa kuomba na kuapta ridhaa ya kimaandishi ya mbunifu wa sanaa husika.

(6) Nakala za mikataba au vibali zitahifadhiwa na Baraza au Kamati inayosusika.

  1. –(1) Maonyesho, mashindano na matamasha ya sanaa yatafanyika baada ya kupata kibali katika kila ngazi kwa utaratibu ufuatao:

(a)    Kwa maonyesho, mashindano na matamasha ya sanaa nayayoshirikisha zaidi ya mkoa mmoja, kibali kitaombwa kutoka kwa Baraza la Sanaa la Taifa

(b)   Kwa maonyesho., mashindano ya matamasha ya sanaa yanayoshirikisha zaidi ya wilaya moja kati ya wilaya za mkoa husika au wilaya isiyo ya mkoa huo, kibali kitaombwa kutoka kwa Kamati ya Sanaa ya Mkoa huo.

(c)    Kwa maonyesho, mashindano na matamasha ya sanaa yanayoshirikisha wilaya moja, kibali kitaombwa kutoaka Kamati ya Sanaa yinayohusika;

(2) Vibali vyote vitatolewa kwa kuzingatia masharti yafuatayo.

      (a)  Shughuli za sanaa zilizoombewa na kupatiwa kibali zitafanyika kwa
            kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo;

     (b) Shughuli za sanaa zilizoombewa na kupatiwa kibali zifanyike bila
           kuwadhalilisha wasanii au dhadhira au kufanya jambo lolote linalokiuka
           maadili na utamaduni wa Mtanzania

     (c) Shughuli hizo zilenge katika kuelimisha, kukosoa, kuburudisha na
          kuhamasisha umma katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii;

(d)   Maombi ya vibali vya maonyesho yawasilishwe kenye ngazi inayohusika si chini ya siku kumi na nne kabla ya siku ya maonyesho

(3) Waandaaji wa maonyesho wazingatie yafuatayo:
     (a) Watoto chini ya umri wa miaka 18 hawataruhusiwa kuingia katika kumbi
          au sehemu zinazouzwa pombe wakati wa maonyesho ya sanaa;

    (b) Mavazi na maleba ya wasanii hayana budi kuwa ya heshima;

    (c)  Sanaa zinazolengwa kwa watu wazima zisionyeshwe kwa watoto
Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


    (d) Watoto wasiruhusiwe kuwepo katika kumbi au maeneo ya maonyesho
          baada ya saa 2.00 usiku

(4) Maonyesho yanaweza kusimamishwa iwapo itabainika kuwa yanakiuka taratibu, kanuni au sheria zilizowekwa, au hayazingatii masharti ya kibali. 

  1. –(1) Kumbi zote za maonyesho ya sanaa zitapangwa kwa madaraja kwa utaratibu ufuatao:
(a)    Daraja A – Kumbi ambazo sauti haisikiki nje
(b)   Daraja B – Maeneo ya wazi ambayo ni maalumu kwa maonyesho ya sanaa
(c)    Daraja C – Kumbi zisizozuia sauti kutoka nje ambazo zimejengwa kwenye makazi ya watu au karibu na hospitali, shule, misikiti, makanisa n.k.

(2) Kumbi zitatumika kwa shughuli za maonyesho ya sanaa kwa utaratibu ufuatao:

      (a)  Kumbi za daraja A zinaweza kutumika kwa shughuli za maonyesho ya
            sanaa wakati wowote kwa kuzingatia masharti ya mamlaka zilizotoa vibali
            vya maonyesho hayo;

     (b)  Kumbi za daraja B zinaweza kuendesha shughuli za maonyesho ya sanaa
           kuanzia saa 10.00 jioni na si zaidi ya saa 5 usiku kwa siku za kuanzia
           Jumatatu hadi Ijumaa. Siku za Jumamosi, Jumapili na sikukuu, maonyesho
           yanaweza kuanza mapema na kumalizika si zaidi ya saa 7.00 usiku

(c) Kumbi za daraja C zinaweza kuendesha shughuli za maonyesho ya sanaa
     kuanzia saa 10.00 jioni na si zaidi ya saa 3.00 usiku kwa siku zote.

  1. –(1) Wasanii au vikundi vya aina yoyote ya sanaa wanaweza kwenda kufanya maonyesho ya sanaa nje ya nchi baada ya kupata kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa. Aidha, vikundi vya maonyesho ya sanaa au wasanii binafsi kutoka nje ya Tanzania wanaweza kufanya maonyesho yao baada ya kupata kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa na mamlaka nyinginezo zinazohusika na uingiaji wa wageni nchini.

(2) vibali vya kwenda nje ya nchi au kuruhusu wageni kufanya maonyesho yao hapa nchini vitatolewa baada ya mwombaji kuthibitisha uwezo wake wa kumudu gharama za uendeshaji wa maonyesho hayo, ikiwa ni pamoja na gharama za wasanii kujikimu wakiwa huko ugenini au hapa nchini.



Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)


  1. ghughuli zote za sanaa zitafanyika kwa kuzingatia sheria ya |Hakimiliki na hakishiriki

  1. –(1) chama, kikundi, asasi au mtu yeyote atakayebainika kuvunja au kukiuka kifungu chochote cha Kanuni hizi anaweza kuchukuliwa hatua zifuatazo:

(a)    Kutozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini (Sh. 50,000/=)

(b)   Kufuatiwa usajili

(c)    Kusimamishwa kuendesha hughuli za sanaa

(d)   Kuzuiwa kujishughulisha na kazi za sanaa kwa kipindi kisichopungua miezi sita

(e)    Kuzuiwa kujishughulisha na kazi za sanaa maisha, kwa kubainika kujihusisha na vitendo vya kupokea au kutoa rushwa.

(2) Adhabu zilizotajwa katika Kanuni ya 31 (1) zinaweza kutolewa mojamoja au kwa pamoja julingana na uzito wa kosa.

  1. Kutakuwepo na ada mbalimbali kwa huduma zitakazotolewa kwa Baraza la Sanaa la Taifa na ngazi zake kama itakavyoonyeshwa katika jedwali iliyomo katika Kanuni hizi.

  1. Baraza, kwa kibali cha Waziri inaweza kurekebisha kanuni hizi kama itakavyoonekana inafaa.















Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa


 
Tangazo la Serikali Na. 322 (linaendelea)
JEDWALI


 
(Kifungucha 32)

ADA ZA HUDUMA

KAMA ZILIVYOREKEBISHWA NA WRAKA WA  WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO, YA TAREHE 16/-7/2009

(Tangazo la Serikali Na. 322 la tarehe 21/10/2005 la Kanuni za BASATA na marekebisho yaliyofanyika kwa idhini ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo ya tarehe 16 Julai 2009)

NA
MHUSIKA
USAJILI
Tsh.
KIBALI
Tsh.
FAINI
Tsh.
1
TAASISI/VYAMA
30,000
50,000

2
PROMOTA/MAKAMPUNI
30,000
200,000

3
WASANII BINAFSI
30,000
40,000

4
VIKUNDI
30,000
40,000

5
FOMU YA USAJILI
5,000
-

6
VIBALI VYA KAWAIDA KUINGIA NDANI YA NCHI
-
1,000,000

7
VIBALI VYA DHARURA KUINGIA NDANI YA NCHI
-
1,500,000

8
VIBALI KUENDESHA MASHINDANO
a.       MASHINDANO YA KIBIASHARA
b.       MASHINDANO YASIYO YA KIBIASHARA

-
-

1,500,000
100,000

9
VIBALI VYA KUENDESHA MATAMASHA:
c.       MATAMASHA YA KIBIASHARA
d.       MATAMASHA YASIYO YA KIBIASHARA

-
-

1,500,000
100,000

10
WAFANYA BIASHARA NDOGONDOGO
30,000
30,000

11
KUMBI ZA MAONYESHO YA JUKWAANI:
a)       Zenye ukubwa wa kukaa watu wasiozidi 350
b)       Zenye ukubwa wa kukaa watu   351 – 550
c)       Zenye ukubwa wa kukaa watu   551 – 750
d)     Zenye ukubwa wa kukaa watu   751 na kuendelea


300,000
500,000
700,000
1,000,000

12
UPOTEVU WA CHETI
-
-
15,000
13
KUBADILISHA JINA LILILOSAJILIWA
-
-
20,000
14
KUTANGAZA/KUENDESHA SHUGHULI ZA SANAA BILA KIBALI CHA BASATA
-
-
500,000
  • Wasanii wanaokwenda nje ya nchi watatakiwa kuomba  kibali cha  BASATA.
               Kibali hiki hutolewa bure.


Dar es salaam                                                                          J.J. Mungai (Mb)
20 Julai, 2005                                                              Waziri wa Elimu na Utamaduni


Certificate of the Permanent National Votgers Register



 


GOVENMNENT NOTICE  NO 323 PUBLISHED ON 21/10/2005

THE PRESIDENTIAL ANDPARLIAMENTARY ELECTIONS
(REGISTRATION OF VOGERS)REGULATIONS, 2004

NOTICE

Made under regulation 31 (3)

CERTIFICATION OF THE PERMANENT NATIONAL VOTERS REGISTER



Citation      1. This Notice shall be cited as the certification of the Permanent
                                  national Voters  Register

Certification 2.-(1) The Director of Elections hebery, certifies that, the Permanent
Of the                     National Voters’ Register shall come into force with effecfrom
register                   1st   October 2005

(2) The Permanent National Voters’ Register shall replace all the Provisional Voters’ Register and shall remain in force until another new register is prepared and certified in accordance with the Regulations.

Made by the Director of Elections this 1st day of October 2005


                            Dar es salaam                                              Rajabu R. Kiravu
                           October, 2005                                           Director of elections














Certificate of the Permanent National Votgers Register



 


GOVENMNENT NOTICE  NO 323 PUBLISHED ON 21/10/2005

THE COUNCILLORS’ ELECTIONS [REGISTRATION OF VOTERS] REGULATIONS, 2004

NOTICE

  Made under regulation 30 (3)


 



CERTIFICATION OF THE PERMANENT NATIONAL VOTERS REGISTER


1. This Notice shall be cited as the certification of the Permanent National     Citation
     voters  Register.

2. –(1) The Director of elections hereby, certifies that, the Permanent            Certification
      National voters’ Register shall come into force with effect from                       of the
      October 2005.                                                                                              registration

     (2) The Permanent National Voters’ Register shall replace all
       The Provisional Voters’ Register and shall remain in force until
       New register is prepared and certified in accordance with the
       Regulations

Made by the Director of Elections this 1st day of October 2005




Dar es salaam                                                                          Rajabu R. Kiravu
October 2005                                                                       Director of Elections

No comments:

Post a Comment