Saturday, January 29, 2011


  Vipaji kutoka mtaani


Leo Tunakuletea jamaa wawili wanaopatikana pande mbili tofauti Mwananyamara na Temeke.Nahisi kama unafill upate kujua walianza lini na wapo wapi sasa!


Wa kwanza anafahamika kwa jina la Wahabi muhidin a.k.a LN


Shaban a.k.a Shebby shine.MPANGO MZIMA


Wasanii hawa ni wasanii wanao jishughulisha na kazi mojawapo ya sanaa ambayo kwa namna moja au nyingine vijana hawa wamejiajiri katika biashara ya muziki wa bongo fleva.


Walianza mziki rasmi mwaka 2000 japo kuwa ilikuwa ki getto getto! Waliweza kupiga tizi la kutosha na unaweza kusema je ilikuwaje ama imekuwaje wasiskike mpaka leo! Hapana jibu ni kwamba wakali hawa wa kitaa walikuwa shule si unajua skuli ndo kila kitu.Ilipo fika 2008 jamaa hawa waliweza kukutana na ku make kundi la watu wa wawili na hapo hapo hawakuchelewa kutuwekea mzigo hewani ambao






unafahamika kama Demu sugar ambao umefanywa katika studio za white record’s chini ya mtayarishaji Stive white.Wasanii hao walipoongea na menejimenti ya blogspot hii waliweka wazi kwa kusema kwa pamoja kama ifuatavyo “Sisi tunafanya mziki kazi na pia ni sehemu ya maisha yetu kwani kila tunapo imba mbele za watu basi kumi kwa mmoja ndio hatatukataa kwa hiyo tunasema kuwa sisi tunakubalika ” nilipo wauliza wanalo la mwisho la kuongezea wakasema kuwa wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau wa mziki na pia ingekuwa freshy kama wangepata na meneja au mtu yoyote atakaye weza kusimamia kazi zao katika mpango mzima wa kurekodi na hata mauzo kwani vijana wana uwezo wa kutosha.
ambao tulikuwa nao katika mahojiano tofautitofauti
kuhusu maisha yao na muziki na hata kitaa panasomekaje,mipango yao.Fuatilia mpango mzima wao katika gemu hii ya bongo fleva na hata kwa yoyote anayehitaji ku dhamini au msaada wa kazi zao studio  piga namba hizi 0713 736 868.

1 comment:

Post a Comment